Welfare of Women | GLOWM

Select Avatar

Select Language

We plan to provide other language versions as soon as funding is available

  • Women's reproductive life stages
  • Painful periods and heavy menstrual bleeding
  • Preventing cervical cancer
  • Understanding breast cancer
  • Respectful healthcare for women
  • Female genital mutilation
  • Preparing for pregnancy
  • Pain and bleeding in early pregnancy
  • Infertility – difficulty in getting pregnant
  • Antenatal care for healthy pregnancy
  • Diet and nutrition in pregnancy
  • Common problems in pregnancy
  • Danger signs in pregnancy
  • Pre-eclampsia
  • Maternal sepsis
  • Premature birth
  • Labor and birth
  • Cesarean section
  • Obstetric fistula
  • Breastfeeding
  • Danger signs in newborn babies
  • Postnatal care
  • Jaundice in the newborn
  • Postnatal family planning (contraception)
  • Menopause
  • Postmenopausal bleeding
  • Bladder and pelvic floor problems
  • Women's health in later years
wow-l2-3-header-logo.png

Contraception

A guide to family planning

An educational
initiative
supported by


Written by experienced doctors, midwives and other medical professionals – and approved by a specialist Editorial Board

Select Avatar

Select Language

We plan to provide other language versions as soon as funding is available

About WoW


Inapakia...

Enhancing the Welfare of Women

Expert Health Information for Women

Nija za Kuzuia Mimba
Mwongozo wa mpango wa uzazi
Uzazi wa mpango hukuzuia kupata mimba wakati hutaki kupata mtoto. Inakusaidia kupanga familia yako ili uweze kusubiri hadi ujisikie tayari kupata mtoto.
Kupanga kupata ujauzito ni muhimu kwani ni salama kwako na kwa watoto wako.
Inasaidia kuzuia watoto wako kuzaliwa kabla ya muda, wadogo sana au ikiwezekana hata kufa.
Watu wengi wana wasiwasi kuhusu njia za uzazi wa mpango, lakini ni salama sana. Ni salama kuliko kupata mimba mapema sana.
Kuna njia nyingi za uzazi wa mpango ambazo zinaweza kutumika kwa kupanga uzazi. Hizi njia zote zinaweza kubadilishwa isipokuwa kuondelewa kizazi.
Njia za kizuizi ni pamoja na kondomu za kiume, kondomu za kike na diaphragm inayotumiwa na dawa ya manii.
Kondomu ndiyo njia pekee inayokusaidia kukukinga dhidi ya VVU na magonjwa mengine ya zinaa iwapo zitatumika kwa usahihi.
Pia kuna njia za muda mrefu zinazoweza kubadilishwa ambazo ni pamoja na:
– IUD (kifaa cha ndani na mji wa mimba) ambazo huingizwa kwenye uterasi
– vipandikizi ambavyo huingizwa kwenye mkono
– sindano zinazotolewa chini au mguu.
Njia hizi ni bora katika kuzuia mimba kuliko njia nyingine. Zinaweza kudumu kati ya miezi 3 kwa sindano na hadi miaka 10 kwa IUD.
Unaweza pia kumeza kidonge cha uzazi wa mpango kila siku ambacho kitakusaidia kukuzuia kupata ujauzito.
Homoni hizi pia zinaweza kuwekawa kupitia kiraka unachovaa katika mkono wako au pete ya uke inayowekwa katika uke. Njia hizi zote ni nzuri sana na salama.
Mbinu ya kufahamu siku za hatari, hufuatilia mzunguko wa hedhi, joto la mwili na ute wa seviksi ili kuonyesha siku ambazo kuna uwezekano mdogo wa kupata mimba.
LAKINI hii SIO NZURI katika kusimamisha ujauzito kama njia nyinginezo na SIYO ya kutegemewa sana.
Kufunga kizazi ni njia pekee ambayo hudumu milele inahitaji operesheni ndogo.
Inajulikana kama vasektomi kwa mwanaume na kufunga kizazi kwa mwanamke.
Kufunga kizazi kunapaswa kuchaguliwa tu ikiwa una uhakika kuwa hutaki watoto wengine zaidi.
Inapopatikana, uzazi wa mpango wa dharura baada ya ngono pia inawezekana. Hii inahitaji unywe dawa maalum au uwe na IUD ya shaba/uweke kitanzi ndani ya siku zisizozidi 5 baada ya kujamiiana.
Uzazi wa mpango wa dharura haupatikani kila mahali.
Baadhi ya njia za uzazi wa mpango zinaweza kuwa na athari zisizohitajika. Kwa Kawaida ni ndogo tu, na hudumu kwa muda mfupi tu.
Hata hivyo, mbinu fulani hutoa manufaa ya ziada, kwa mfano baadhi zinaweza kusaidia kwa damu nyingi za hedhi au yenye uchungu.
Muulize mhudumu wako wa afya kuhusu mbinu zinazopatikana na lini na jinsi gani unaweza kuzipata.

Mwandishi wa programu hii ya CONTRACEPTION ni:

  • Dk Anna Graham
    King's College Hospital NHS Foundation Trust, London, Uingereza

Mpango wa Ustawi wa Wanawake umeundwa chini ya Uhariri Mkuu wa Dk Kate Lightly, Chuo Kikuu cha Liverpool, Uingereza na unasimamiwa na Bodi ya Wahariri ya Kimataifa

Gharama ya kuzalisha nyenzo hii imefadhiliwa kwa sehemu na ruzuku ya elimu kutoka GSK

/